Diamond Platnumz na Wema Sepetu ni miongoni mwa mapenzi yaliyokuwa kwenye midomo ya Watanzania wengi kutokana na watu wengi kuvutiwa na ‘Couple’ hiyo na wengine mpaka sasa wanatamani kuona wawili hao wakiwapamoja,mwishoni mwa mwaka 2014 waliingia kwenye headlines za kuachana na kila mmoja kuendelea na maisha yake.
Platnumz kwa sasa yuko na Zari huku Wema Sepetu akiwa na mshindi wa Big Brother 2014 Idris Sultan,toka Diamond na Wema Sepetu kuachana tumesikia mara kadhaa wakiripotiwa kuwa hawaelewani,lakini July 05 Diamond Platnumz ameamua kuonyeshesha kuwa hawana tofauti kwa kupost tangazo la show ya Christian Bella na Idris Sultan show ambayo inasemekana imeandaliwa na Wema Sepetu.
Siku kadhaa Wema Sepetu ameonekana akijirekodi akiimba nyimbo za Diamond Platnumz kwenye mtandao wa Snapchat.
Post a Comment