0
Wizkid adaiwa kuingia kwenye mahusiano na meneja wake
Wizkid amewaacha mashabiki wake kwenye mabano baada ya kuwepo kwa taarifa za chini kuwa ameingia kwenye mahusiano mapya na meneja wake wa nchini Uingereza, Jada.
Picha aliyopost Wizkid akiwa na Jada kwenye akaunti yake ya instagram ndiyo iliyoongeza maswali zaidi baada ya kuandika, “@__jada.p forever my G!! 💥.”
Neno G aliloliandika Wizkid kwenye picha hiyo limetafsiriwa na wengi kwa kirefu cheke kuwa ni ‘Girlfriend’ japo humaanisha pia ‘Gangster.’ Ni muda mrefu staa huyo hajayaweka mahusiano yake wazi tangu alipoachana na aliyekuwa mpenzi wake, Tania Omotayo.









Post a Comment

 
Top