Jana Ijumaa (May 23) Kanye West na Kim Kardashian
waliianza ratiba yao kuelekea siku ya harusi ya mwaka inayosubiriwa kwa hamu
kubwa kwa kufanya ‘pre-wedding dinner party’ huko Paris, Ufaransa huku ndoa
yenyewe ikitarajiwa kufungwa leo.
Maharusi Kim Na Kanye wakiongea mbele ya wageni waalikwa
Jana mitaa ya Paris ilishuhudia pilikapilika za wageni na
mapaparazi wakielekea eneo ilipofanyika sherehe ya chakula cha jioni kabla ya
ndoa (pre-wedding dinner), iliyohudhuriwa na wageni wanaokadiriwa kufikia 100
wakiwemo dada zake Kim, Kourtney, Khloe, Kylie, Kendall na mama yake Kris
Jenner na wageni wengine mbalimbali.
Usiku huo ulipambwa na burudani mbalimbali ikiwa ni
pamoja na mwimbaji aitwaye Lana Del Rey.
Kwa mujibu wa ripoti, fataki zilitawala eneo la tukio,
huku ikisemekana anga la eneo hilo siku ya jana lilikuwa ‘NO-FLY ZONE’, hakuna
ndege yoyote iliyokatiza.
Chupa 1,000 za champagne ziliandaliwa kwaajili ya wageni
waalikwa waliohudhuria.
Kwa mujibu wa Entertainment Tonight, maharusi watarajiwa
Kimye waliwatangazia wageni waalikwa kuwa ndoa yao itafungwa siku inayofuata
yaani leo Jumamosi (May 24) huko Italy.
ASANTE KWAKUTEMBELEA WEBSITE HII JIUNGE NASI KUWA MWANA FAMILIA WA JIMMCARTER.COM FACEBOOK-JIMCARTERTZ | TWITTER JIMMCARTERTZ
Post a Comment