0
Chelsea wamekubali kumuuza beki David Luiz kwa takriban paundi milioni 40 kwenda kwa mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain. 
Luiz alijiunga na Chelsea kutoka Benfica Januari 2011 kwa paundi milioni 21.3. 

"Uhamisho huo sasa unasubiri David Luiz kukubaliana masuala binafsi na PSG na pia kufanyiwa vipimo vya kiafya" imesema taarifa kwenye tovuti ya Chelsea. 
Luiz amekuwa akinyatiwa na Barcelona kwa misimu miwili iliyopita, lakini PSG wameamua 'kuvunja benki' na kumfanya beki aghali zaidi duniani.
ASANTE KWAKUTEMBELEA WEBSITE  HII JIUNGE NASI  KUWA MWANA FAMILIA WA JIMMCARTER.COM FACEBOOK-JIMCARTERTZ | TWITTER JIMMCARTERTZ

Post a Comment

 
Top