Uhuru wa Chris Brown kwa sasa bado ni
ndoto sababu Ijumaa iliyopita (May 9) jaji wa mahakama ya Los Angeles
alimhukumu mwimbaji huyo kifungo cha mwaka mmoja jela (siku 365), baada ya
kukiri kuvunja masharti ya kesi yake ya kumpiga aliyekuwa mpenzi wake Rihanna
mwaka 2009.
Jaji anayeisikiliza kesi hiyo, James R.
Brandlin alimuondolea siku 234 za kifungo hicho ambazo tayari amezitumikia kwa
kukaa rehab na jela, hivyo anatakiwa kumalizia siku 131 zilizobaki.Breezy aliwekwa jela toka katikati ya
March baada ya kuvunja sheria za rehab huko Malibu, alipoamriwa kukaa kwaajili
ya matibabu ya kukabiliana na hasira.Kesi zinazomkabili mwimbaji huyo wa
R&B kwa kiasi flani zimeathiri muziki wake japo management yake inajitahidi
kuendelea kutoa nyimbo mpya akiwa jela.
Mwezi March aliachia video ya version
ya tatu ya wimbo wake ‘Loyal’ aliyowashirikisha Lil Wayne na Tyga, na mwezi
uliofuata (April 15) aliachia video ya moja ya nyimbo zitakazokuwepo katika
album yake ya ‘X’, “Don’t Be Gone Too Long” aliomshirikisha Ariana Grande.Mwezi February mwaka huu Brown
alitangaza tarehe mpya ya album yake kutoka (May 5) ambayo imemkuta jela. Album
hiyo imeahirishwa mara kwa mara toka mwaka jana kutokana na sababu mbalimbali.
Post a Comment