Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa
(Fifa), Sepp Blatter ametangaza kwamba atatetea nafasi yake kwenye uchaguzi
ujao mwakani.
Blatter alikuwa akidhaniwa kwamba
angestaafu na tayari wanamichezo wengine walianza kufikiriwa kuchukua nafasi
yake, lakini amekata mzizi wa fitna akisema anagombea kwa mara ya tano.
Blatter aliliambia gazeti la nchini
mwake Uswisi la ‘Blick’ kuwa bado ataitaji muda zaidi ya kwakuwa bado ajamaliza
majukumu yake.
“Mimi ni mgombea wa nafasi hii tena.
Muda wangu unamalizika lakini kazi yangu niliyotaka kufanya bado,” alisema
Blatter
Uchaguzi huo utafanyika katika makao
makuu ya shirikisho hilo, Zurich nchini Uswisi Juni mwakani.
Makamu wa Rais wa Fifa, Jeffrey Webb na
aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Jerome Champagne wamekuwa wakitajwa kama mbadala
wa Blatter lakini wote wamesema kwamba hawatasimama kushindana na rais wa sasa.
Kiongozi wa Uefa, Michel Platini anadaiwa kutaka kumng’oa Blatter hapo Fifa,
ili aingize mipango mipya.
Post a Comment