0

  Dr Dre Asherehekea kuwa bilionea wa kwanza kwenye hip hop, 
Forbes wasema ‘bado kwanza’
  Wakati ambapo Dr Dre na washkaji zake akiwemo Tyrese wameangusha party kusherehekea, Forbes wamesema Dre hatakiwi kuanza kuhesabu kuku wake kabla hajawataga – yaani kujiita bilionea wa kwanza kwenye Hip Hop. 

 Forbes imeuambia mtandao wa TMZ kuwa baada ya Apple kukamilisha malipo yake ya dola bilioni 3.2 kuinunua kampuni ya Beats Electronics, rapper na producer huyo hatofikisha kiwango cha dola bilioni moja.  Mhariri Msaidizi wa Forbes wa masuala ya fedha, amesema wamefanya hesabu na na baada ya kodi na vitu vingine, Dre atakuwa na utajiri wa dola milioni 800. 
Imeonekana kuwa Dre anamiliki asilimia 25 tu za kampuni hiyo


ASANTE KWAKUTEMBELEA WEBSITE  HII JIUNGE NASI  KUWA MWANA FAMILIA WA JIMMCARTER.COM

Post a Comment

 
Top