Mwigizaji na mwongozaji wa filamu Tanzania Adam Philip Kuambiana amefariki dunia alfajiri ya kuamkia leo (May 17). Kwa mujibu wa GP Kuambiana amefariki wakati akipelekwa katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es salaam, baada ya kudondoka chooni akiwa location katika hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remmy. Inadaiwa kuwa kabla ya umauti kumfika marehemu Kuambiana alikuwa akilalamika kusumbuliwa na tumbo. Tunawapa pole wana bongo movie, ndugu, jamaa na marafiki kwa kumpoteza Kuambiana.
Mungu Ailaze Roho Ya Marehemu Mahala Pema, Amen.Mbele Yeye Nyuma Yake Sisi
Post a Comment