0

 Kiwanda cha filamu nchini, kimepata pigo jingine baada ya kuondokewa na muigizaji na mtayarishaji wa filamu wa kike aliyekuwa anakuja juu, Rachel Haule. Rachel amefariki jana baada ya kujifungua kwa upasuaji.
Rachel alikuwa mjamzito… Na taarifa niliyoipata tangu jana ni kwamba kulitokea complications wakati wa kujifungua ambapo alijifungua kwa operation mtoto akafariki na yeye akawa amelazwa icu.. Lakini asubuhi ya leo mungu akamchukua na yeye…. Hivyo ni mama na mtoto ambao wamepotea.. Pole sana Saguda kwa msiba huu mkubwa wa kupoteza mama na mtoto,!!!!! Kazi ya mungu haina makosa,” ameandika Zamaradi Mketema kwenye Instagram.

“Jana alifanikiwa kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya uzazi baada ya hapo hali yake haikuwa nzuri aliwekwa katika chumba cha wagojwa mahututi, kwa bahati mbaya leo asubuhi ameaga dunia,”rafiki yake wa karibu aliuambia mtandao wa Filamu Central.
Rachel aliigiza kwenye filamu mbalimbali zikiwemo Vanessa in Dillema na Men’s Day Out. Kifo chake kimekuja siku chache baada ya muongozaji na muigizaji wa filamu Adam Kuambiana kufariki dunia. Msiba huo umepokelewa kwa majonzi na mastaa mbalimbali nchini.
Shilole
Staki kumkufur mwenyez Mungu wangu! Ila kazi yake haina makosa tulimpenda ila mwenyezi Mungu kampenda zaid! Dah inauma sana pole Saguda kwa mtihan uliokupata!Ila tupo pamoja kwa kipind hik kigumu 1h
Zamaradi Mketema
OMG!!! Sijawahi kushtuka kama hivi… nasikitika kutangaza MSIBA mwingine mkubwa ndani ya BONGO MOVIE!!! RACHEL HAULE hatunae tena duniani… AMEFARIKI Asubuhi ya leo… INALILLAHI WAINAILAIHI RAJIUN…. pumzika kwa Amani mama… MUNGU YUPO jamani!!!!! 2h
Jacky Wolper
Recho haule me nakutambua kma sheilah kipnd ni rafk yangu kipenz nilikua napenda kukuita sheila .R.i.p sheilah umeamua kumzalia mwanaume unaempenda saguda lkn aikufanikiwa mtoto akaiga dunia na sasa umefwata wewe jaman ni pigo kubwa kwakijana yule na kwa famly na sisi bongo movie pia..Mungu amekupenda zaidi ..pole saguda shemeji yetu…R.I.P sheilah 8min
Riyamaally
Innalilahi wainna ilaihirajiun mbele yako nyuma yetu kazi ya mungu hainamakosa kila nafsi itaonja umauti mungu akuweke unapo stahili maa amen daima tutakukumbuka na pengo lako halitafutika kamwe pumzika kwa amani pole sana kaka saguda mungu akujalie sunira na uvumilivu amin pole familia pole bongo muvi na tuwe pole kwa sote kila alie guswa na msiba huu jamaa na marafiki ,,,,natue pole kwa sote kazi yake mola daima haina makosa mungu ameleta nae amechukua jina lake lihimiliwe milele amin 5min
Batulli
batuli_actress Alhamdulilah……Innalilah Wainnailah Rajouun “Yarabbi Tupe Subira, Yarabbi Tupe UvumilivuASANTE KWAKUTEMBELEA WEBSITE  HII JIUNGE NASI  KUWA MWANA FAMILIA WA JIMMCARTER.COM FACEBOOK-JIMCARTERTZ | TWITTER JIMMCARTERTZ 

Post a Comment

 
Top