0
Jina la Aliaune Damala Badara Thiam labda ni gumu kumjua huyu ni staa gani wa muziki duniani.. okay, jina lake kwenye stage ni Akon, Msenegal aliyetoboa anga na kufanikiwa kutengeneza mafanikio makubwa kupitia muziki duniani akiwa kwenye ardhi ya Marekani !!

Akon alikuwa Kenya mwezi mmoja uliopita kwenye fainali za Trace Music Star, ikawa furaha kwetu kumuona Mayunga wetu kaibuka mshindi.. safari inaendelea kati ya Mayunga na Akon kwenye muziki, tutarajie chochote kikubwa zaidi kupitia kinachoenda kufanyika marekani.
Ishu ambayo nimeona nikusogezee ni kuhusu Akon mwenyewe.. kwa sasa jamaa kaamua kuwekeza mamilioni ya pesa zake kwenye miradi ya solar energy Africa, watu zaidi ya milioni 600 watanufaika na mradi huu.
Ndani ya mwaka mmoja nchi ambazo zitakuwa zimeshanufaika na mradi huu ni Mali, Guinea, Benin, Senegal, Niger, Gabon, Equatorial Guinea, Congo-Brazzaville, Kenya, Sierra Leone na Burkina Faso.
Mradi huu umepewa jina la Akon Lighting Africa,

Post a Comment

 
Top