Ikiwa leo ndio Ligi kuu ya Uingereza inaisha huku timu ya Chelsea wakiwa mabingwa wa msimu huu, mshambuliaji wa klabu hio Didier Drogba amefanya maamuzi magumu juu ya maisha yake ya soka na klabu hio.
Mashabiki wa Chelsea watakuwa na furaha na huzuni baada ya kuwa mabingwa na kumpoteza Drogba ambaye ametangaza kuiacha klabu hio na kwamba hii ndio mechi yake ya mwisho.
Drogba aliandika ujumbe huu kupitia Instagram kuwa ” Nimezungumza na kocha wangu Jose Mourinho kuhusu hatma yangu kuwa nataka kuendelea kucheza soka hata msimu moja na ili nicheze zaidi soka lazima niende timu nyingine”.
Drogba anamiaka 37 alijiunga kwa mara ya kwanza na Chelsea mwaka 2004 na ameifungia magoli 104 kwenye mechi 253 za ligi.
Post a Comment