Msimu wa Christmas na Mwaka Mpya ndio huu umeanza mtu wangu zikiwa zimebaki siku 23 kufikia December 25.
Wasanii mbalimbali Marekani wamejitokeza kutoa nyimbo kwa ajili ya msimu wa Christmas na miongoni ya hao wasanii ni Chris Brown.
Nimetembelea Instagram page ya Chris Brown na huko nimekutana na post yake moja inayosema, mauzo ya Album yake mpya, Royalty yatatumika kuwezesha vituo vya watoto yatima kuendesha shughuli zao msimu huu wa Christmas na Mwaka Mpya.
Kila dola 1 (ambayo ni sawa na Tzs. 2000 ya nyumbani) itakayopatikana kwenye mauzo yote ya nakala za pre-order yatakusanywa na kuwekwa kwenye mfuko wa Children’s Miracle Network na mfuko wa Shirika la Best Buddies kwa ajili ya kuwezesha sikukuu yao ya Christmas kwa mwaka huu
Kupita Instagram page yake @chrisbrownofficial, Chris ameandika “Pre-order #ROYALTY sasa hivi & dola 1 kutoka kwenye kila copy ya Album iliyouzwa itatumika kusaidia @CMNHospitals & @BestBuddies! Happy Holidays!“ @chrisbrownofficial.
HII HAPA ORODHA YA NYIMBO KATIKA ALBUM YA ROYALTY
ROYALTY TRACKLISTING
1. “Back to Sleep”
2. “Fine By Me”
3. “Wrist” feat. Solo Lucci
4. “Make Love”
5. “Liquor”
6. “Zero”
7. “Anyway”
8. “Picture Me Rollin'”
9. “Who’s Gonna (NOBODY)”
10. “Discover”
11. “Little Bit”
12. “Proof”
13. “No Filter”
14. “Little More (Royalty)”
DELUXE EDITION
15. “Day One”
16. “Blow It In the Wind”
17. “KAE”
18. “U Did It” feat. Future
Post a Comment