Flaviana Matata, Jumatano hii amezindua bidhaa yake ya urembo wa kucha iitwayo Lavy.
Akizungumza na waandishi wa habari katik Saloon ya ‘Pikasso Beauty and Spa Saloon’ iliyopo Posta jijini Dar es salaam, Flaviana alisema anashukuru Mungu ameweza kutimiza ndoto yake ya muda mrefu.
Flaviana akizungumza na waandishi wa habari
“Nashukuru Mungu kwa kweli hii project nilianza kushughulikia miaka miwili iliyopita,” alisema.
“Kwenye launch ya leo nimelenga kuwaalika watu ambao wana maduka ya vipodozi na saloon pamoja na marafiki zangu.
Kwa maana naamini ukithamini wateja wako hao ndio watakuwa watu wangu wa muhimu. Kwahiyo bidhaa yetu inaingia sokoni na bei ya reja reja itakuwa shilingi 5000 na kwa sasa zitapatikana pale Shear illusions, Picasso pamoja na Zuri Cosmetics. Pia kadri tunavyoendelea na jinsi watu wanavyozidi kuomba oda ndivyo zitakavyoenea kila sehemu.”
Pia Flaviana alizungumzia ubora wa bidhaa hiyo pamoja na mpango wa kuongeza bidhaa nyingine sokoni.
Flaviana Matata akiwa na mtu wake wa karibu
“Kuna chemical haziruhusiwi kwenye ‘nail polish’. Kila unapotaka kuanzisha product kuna muongozo unapewa. Pia kikubwa zaidi ni ubora wa bidhaa wa kuweza kukaa kwenye kucha kwa muda mrefu. Hii ni rangi ya kawaida sio jelly, inakaa siku tano mpaka saba. Kwa sababu tayari nilisambaza kwa rafiki zangu na wamelishuhudia hilo.”
Flaviana Matata na Nancy
Post a Comment