0

 Diamond Plutnumz  ameamua kufunguka nakuwaelewesha watu  wanaosema kuwa video yake mpya ya wimbo wa make me sing
alioshirikiana na rapper AKA kutoka Afrika kusini unafanana na video ya Got money ya Lil wayne.

Plutnumz  amethibitisha ule usemi wa hakuna jipya chini ya jua kwa kusema kuwa hakuna mtu yeyote atayefanya kitu kwenye muziki ambacho hakijafanyika.

“Watu wanashindwa kuelewa,kila kitu ambacho kinafanyika sasa hivi kwenye muziki kuanzia video,mashairi vyote vilishafanyika,vyote vilishaimbwa ,ni kama vinafanyika kwa marudio lakini kila mtu anarudia kwa namna yake anayoijua yeye,kwa sababu ukisema nakupenda watu washaimba,sikupendi washaimba vyote yaani” maneno ya Platnumz 

Kwasasa video hiyo ilefikisha Viwes mlioni moja ndani ya siku kumi tangu kutoka na kufanya msanii AKA kuwa msanii wakwanza South africa Kufikisha Watazamaji milioni moja ndani ya siku kumi


Post a Comment

 
Top