Diamond, Nay wa Mitego na Alaine wa Jamaica waingia studio kutayarisha wimbo
Diamond Platnumz, Nay wa Mitego pamoja na msanii mwana dada wa Jamaica, Alaine wameingia studio kwa kile kinachoonekana kama kurekodi wimbo kolabo.
Bado haijulikani ni nani amemshirikisha nani lakini kuna uwezekano mkubwa Alaine amemshirikisha Diamond.
Na Nay wa Mitego ameshare picha Instagram akiwa studio pamoja na Diamond, Alaine, Tudy Thomas, meneja wa Diamond, Sallam na wengineo.
Mwana dada Alaine amekuja Afrika Mashariki wiki iliyopita na anatarajiwa kuzindua album yake mpya nchini Kenya.
Ni Kwamara ya pili muimbaji huyo wa jamaica anakuja nchini. Mwaka 2013 alikuja kwenye Fiesta ya Dar es Salaam.
Post a Comment