Mshambuliaji wa Real Madrid @cristiano Ronaldo amekuwa mwanamichezo wa kwanza duniani kutimiza idadi ya mashabiki millioni 200 kwenye social media.
Ronaldo ambaye alikuwa binadamu wa kwanza kutimiza mashabiki millioni 100 kwenye mtandao wa Facebook miezi kadhaa iliyopita – na mpaka sasa anao 109.7 million followers kwenye Facebook, 49.6 million kwenye Instagram na 40.7 million katika mtandao wa Twitter.
Mpinzani wake wa kwenye soka @leomessi anamfuatia kwa mbali akiwa wafuasi million 122.
Namba za Ronaldo zinamfanya aipite idadi ya jumla ya namna za mastaa wa basketball LeBron James, Michael Jordan, Kobe Bryant, Kevin Durant na Steph Curry, ambao jumla yao wana mashabiki 187 million.
Mwaka 2015, Ronaldo alipata followera wapya 41.8 million huku robo 3 ya hao wakitokea instagram. Ana wastani wa kupata followers 135,000 kwa siku.
Faida mojawapo anayopata Ronaldo kwa kuwa na wafuasi wengi kwenye mitandao ni kupata dili nono za matangazo ya biashara.
Post a Comment