0

Dada wa merehemu mwanamuziki Prince ajulikanae kwa jina la Tyna Nelson aliweka wazi hususani mazishi ya mwamamuziki huyo baada ya watu na mashabiki mbali mbali kuanzisha ibada zao za maombolezo ya marehemu Prince.
 Prince alifariki mwishonI mwa mwez wanne akiwa na umri wa miaka 57.
Dada yake na marehemu alieleza kua yeye pamoja na familia yake hawahusiani na ibada iliyoandaliwa na kanisa  ambalo alikua akihudhulia marehemu Prince, na wala hakuna atakaye jishughulisha na ibada hiyo.
Tyna Nelson alisema “ Sio mimi au mabaki ya kaka yangu yatashiriki katika ibada yeyote ya mazishi” 
Kanisa la Mashahidi wa Jehovah lililopo mji wa Minnetonka, Minnesota liliandaa ibaada maalumu kwa ajili ya marehemu Prince kwani alikua akisali hapo enzi za uhai wake.

Tyka Nelso alihamia na facebook na kuandika post ya kushukuru kwa wote walioandaa ibada kwa ajili ya kumuaga kaka yake huyo, na kusisitiza kua ibada hizo zote zinazowekwa sio maalumu kwa ajili ya mazishi ya kaka yake.
Alimalizia kwakusema ibada ya kumuomboleza kaka yao mpendwa inaweza ikafanyika mwezi wa nane na kusema kua “wanahisi kusherekea maisha ya marehemu kivingine na kitofauti sana”

Post a Comment

 
Top