Kulingana na tuhuma za shabiki ambaye kwa sasa anataka zaidia ya millioni nne kwa ajili ya matatizo yake, mwanamuziki Chris Brown ajikuta akishtakiwa kwa wizi wa kofia na shabiki wake.
Kwa mujibu wa kesi iliyoripotiwa mahakamani na mtu ajulikanae kwa jina la Marq Stevenson, amaweka madai ya kuhudhuria tamasha la Chris Brown lililofanyika mwaka jana huko mjini Dallas, Marekani na kumpa kofia moja ya “lackey” (muhudumu au mfanyakazi) wa Chris Brown ili mwanamuziki huyo atie saini katika kofia hiyo kama alama ya kumbukumbu.
Marq Stevenson anasema baada ya hapo hakupata hiyo saini na wala kofia yake hakurudishiwa. Katika mashtaka aliyopewa Chris Brown, Stevenson alilalamika kutopokelewa vizuri na kuonewa na wafanyakazi hao wa Chris Brown. Sasa mtoa mashtaka anasema kofia yake imeibiwa na anataka fidia ya kofia hiyo inayosemekana kununuliwa kwa kiasi cha $25 tu.
Sio hivyo tu, anataka $225 aliyotumia kununua ticket kwa ajili ya tamasha hilo, pia ameomba kulipwa $2,500 kama faini ya uonevu aliyofanyiwa.
Kwa ujumla kwa sasa kofia hiyo itamghalimu Chris Brown karibu millioni tano na nusu ($2,750). Mtoa mashtaka hana shida tena ya saini, bali anataka hela tu.
Post a Comment