0

Mtu mmoja alionekana kua na issue na mgombea uraisi wa Marekani  Donald Trump, au Zaidi hasa labda huyo mtu alikua na issue na hoteli inayomilikiwa na mgombea huyo. Mtu huyo asiye julikana jina aliweza kupanda na kufika ghorofa ya saba ya hoteli hiyo na kutishia kuruka. 

Inasemekana pia mtu huyo alikua na mzozo Fulani juu ya maswala Fulani katika hoteli hiyo. Walizi walimuomba mtu huyo kushuka na kuondoka lakini badala yake akaenda mwishoni mwa jengo hilo ikiwa ni karibu na kutaka kudondoka ili kuonyesha kua alikua anamaanisha kuhusu swala la kutaka kuruka. 

Alikaa juu ya ghorofa hiyo kwa masaa saba akiwa anatishia kuruka lakini baadae aliamua kushuka, na mapolisi wakamchukua na kumpeleka kufanyiwa uchunguzi wa akili.
Bofya Play Kutazama Tukio Zima 

Post a Comment

 
Top