Mwanamuziki Jason Derulo alithibitisha kuachana na mpenzi wake Daphne Joy Jumanne hii katika chanzo cha habari cha “Page Six”. Wawili hawa walikutana Uingereza na baadae walianzisha mahusiano yao mwishoni mwa mwaka jana ambapo walionekana pamoja katika ufukwe wa bahari ya “Miami” huko Marekani.
Pia wakaonekanana pamoja mwezi wa kwanza wa mwaka huu katika “red carpet ya ‘The people’s Choice awards’. Daphne ndo inasemekana kua amevunja uhusiano wao lakini kuachana kwao kulikua ni kwa kiamani, hakuna ugomvi kati yao.
Kabla ya wawili hawa kua na mahusiano, Jason Derulo mwenye miaka 26, alikua na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Jordin sparks na wakadumu kwa miaka mitatu. Walikuja kuachana mwezi wa nne 2014. Pia Daphne Joy mwenye miaka 29, ni mama wa mtoto mmoja aitwae Sire, na alizaa na mwanamuziki 50 cent. Jason alitafutwa kuelezea zaid juu ya kuachana kwao lakini hakua na la kuongea Zaidi.
Post a Comment