Bongo Kwa sasa ukizungumzia wale watu maarufu ambao wana trend sana kwenye mahusiano yao basi hapa utamzungumzia penzi jipya la Harmonize kutoka WCB pamoja na star wa bongo movie Jackline Wolper.
Jackline Wolper amejibu swali ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza Diamond platnumz anachukuliaje mahusiano yake na Harmonize ambaye yupo chini ya Diamond platnumz na ikiwa kipindi cha nyuma mrembo huyo alishakuwa na mahusiano na Platnumz
Akizungumza kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV kinachofanywa na Zamaradi Mketema, Jackline Wolper alisema haya .....
“Diamond rafiki yangu sana ni mtu ambae nategemea hata kuja kufanya nae filamu, Diamond ni rafiki yangu sana licha ya watu wanaweza wasielewe, lakini sasa hivi Diamond ni baba mkwe wangu,
“kuhusu Harmonize nampenda kwa sababu ana hofu ya mungu, ana heshima sana mwisho hawezi kufanya maamuzi bila kuomba ushauri, katika kunipenda mimi alipiatia pia kuomba ushauri kwa Diamond ambaye ni boss wake kaka yake na kupewa ruhusa kwa hiyo Baraka zimetoka kwa Diamond mwenyewe”
Post a Comment