0

Kuna taarifa sinazosambaa kua malkia wa label ya Mavin Records chini ya mwanamuziki Don Jazy, Tiwa Savage anategemea kuingia mkataba mpya na label ya mwanamuziki Jay Z inayojulikana kama “Roc Nation”. 

Kwa sasa Tiwa Savage anapewa uangalizo wa karibu sana na Jay Z na yupo tayari kuingia mkataba na malkia huyo wa Mavin Records chini ya labe yake hiyo ya Roc Nation.
Kwa mujibu wa vyambo mbali mbali vya habari Nigeria  vinasema kuwa Jayz ameonekana kushangazwa na wasifu wa mwanandada huyo na aliamuru kuanzisha taratibu hizo za kumuingiza Tiwa Savage katika label yake  akiwa na Briant Biggs na Shawn Pecas.

Roc Nation ni label kubwa huko Marekani ikiwa inafanya kazi na wasanii wakubwa kama Rihanna, Big Sean, Dj Khaled, J.cole na wengine wengi tu.

Tiwa tayari ameshapangiwa kufungua katika tamasha la Rihanna litakalo fanyikwa mwezi wa tisa mwaka huu huko Marekani. Na kwasasa hiki ndicho anachokihitaji mwanadada huyo hususani baada ya kua kwenye matatizo na ndoa yake.

Bado tunasubiri uthibitisho juu ya hiki kinachosemekana kinaendelea kutoka kwa muhusika mwenyewe Tiwa Savage.

Post a Comment

 
Top