Ni karibia miaka miwili sasa tangu mwanadada Nicki Minaj aachane na bwana ake wa zamani Safaree Samuels lakini cha kushangaza bado wana migogoro ya hapa na pale.
Usiku wa Jumanne May 10 Nicki Minaj aliweka hadharani tweet inayohusu bwana ake huyo kumshataki na kudai alikuwa akinyanyaswa kihisia na kijinsia na msanii huyo katika kipindi chote cha miezi 11 ya mahusiano yao.
Nicki aliongezea na kuandika kwenye tweet hiyo kua Ex wake anaharibu maisha yake kwa kujaribu kutumia umaarufu na uwezo aliyonao ili alipe faini kubwa.
Nicki Minaj ameahidi kutumia sheria na kumshtaki Ex wake huyo kwa kosa la kutaka kumuibia kwa njia ya kumtafutia kesi isiyokua na vithibitisho vyovyote dhidi yake.
Unaweza kusoma hizi tweet za Nick Minaj
SAFAREE KAMA HAKUKA KIMYA ALIJIBU HIVI
Story By: Eye De Marie
Post a Comment