0

“JAY Z NA BEYONCE WATENGENEZA ALBUM YA SIRI  BAADA YA ILE YA ‘LEMONADE’ “
Beyonce & Jay Z wanatarajia kuachia album ambayo inasemekana kua ni “surprise” kwa wengi kwani hata baada ya “cheating drama” (drama za usaliti) katika album ya “Lemonade” wa wili hawa bado wapo katika penzi moto moto. 

Taarifa zina sema kua wawili hawa wamesha fanya album pamoja na wanatarajia kuiachia hivi karibuni. Album hiyo inatarajia kujibu maswali mengi ambayo yamekua yakiwaumiza watu kichwa kutokana na album ya “Lemonade”.

Sahau kuhusu wawili hawa kuachana, Beyonce mwenye miaka 34, na Jayz akiwa na miaka 46 wanataka kutawala hili game la ku rap wakiwa kama “malkia na mfamle”. 
Licha ya kwamba malkia Bey aliachia ladha mbali mbali katika album yake mpya ya “Lemonade” akimshutumu mume wake kumsaliti, wana hip hop hawa waliobatizwa majina kama “Bonnie na Cylde”  wamejipanga kwa kuja na album hiyo mpya waliofanya pamoja.

Album ya “siri” ya  wawili hawa inasemekana imeshakamilika vyanzo vya habari viliiambia tovuti ya “page six” na inatarajiwa kuachiwa hivi karibuni.Taarifa zinasema kwamba Album ya wanandoa hawa imetengenezwa kama mwitikio na kujibu mashambulio aliyokua akipewa mwanadada Beyonce baada ya kuachia album yake ya “lemonade”

Vyanzo vya habari viliiambia “page six” kua “Jay na Beyonce wasingekua tayari kamwe kwenda kufanya mahojiano na kujibu maswali yote yanayoulizwa,ila ni kawaida yao kujibu kwa kupitia music”

Bado haijulikani ni muda gani Bey na Jay wamekua wakiifanyia kazi album hii, kwani Bey yupo katikati ya ziara yake ya music  ambayo aimeipa jina la “Formation Tour”.Jayz nae anasemekana kua “busy”, ambapo alionekana katika tamasha la mwimbaji mwenzake Puff Daddy huko Brooklyn Barclay’s Center mnamo tarehe 20 mwezi huu wa tano.Ilikua ni muunganiko wa “Bad boy family”.

Jay z aliripotiwa kufanya album yake mwenyewe ya “Lemonade” akiijibu juu ya uvumi aliopewa wa kumsaliti Bey kwa kutembea na “Becky with the good hair” (Becky mwenye nywele nzuri”.

 Album ya Jayz (jaymonade? Lemonjayde?) ingeinua watu wengi sana na kuonyesha watu kwamba “kuna wanaume wema wengi tu duniani” chanzo cha habari cha hollywoodlife kilitoa dondoo hizo. Rekodi hiyo isingekua ya kumkashifu Beyonce bali ingekua ya “kusifu na kuwaheshimu wale wanaume na wa baba wema waliopo duniani” hivyo ndivyo ilivyokua ikizaniwa.


BY :Eye De Marie

Post a Comment

 
Top