Mwanadada Kim Kardashian ambae pia amekua mke wa mwanamuziki Kanye West,ameonekana kuchoshwa na vituko vya mume wake huyo wa miaka miwili. Wanandoa hawana wanasemekana kua walikua wakilala vitanda tofauti tofauti kwa takribani miezi tisa sasa.Na sio hayo tu, inasemekana wamekua wakigombana hapa na pale na vituko vya Kanye West vimemfika shingoni Kim Kardashian.
Ripoti inasema kua dollar billioni moja ($1 billion) inaweza ikamtoka mwanamuziki Kanye West katika kuachana kwao.
Chanzo chetu cha habari cha KUWTK,kina sema kua mwanadada Kim amejiandaa vya kutosha katika kuachana kwao na amepanga kumkomesha Kanye West kwani amekua akimpelekesha sana kuanzia nguo za kuvaa, vitu vya kufanya, mpaka mambo ya kitandani.
Kim ameonekana kuchoka na kupelekeshwa kwake kwani licha ya hayo yote, wamekua wakigombana hapa na pale na kuto kua na maelewano kabisa kama wanandoa. Ameamua kuvua manyanga kwa kumuacha Kanye.Tabia za Kanye zimekua zikimchosha Kim kila siku na hivyo ameamua kuondoka kabla mambo hayajawa mabaya Zaidi.
Wanandoa hawa wamekua wakigombana kupita kiasi, ripoti zinasema..hususani ni kwasababu Kim Kardashian amechoshwa na vituko vya mume wake huyo kwani vinamtia aibu sana. Kanye amekua akijifanya kama Mungu kwa Kim. Mfano mzuri walitakiwa kwenda katika mji wa Cannes mwaka huu, lakini walianza kubishana kabla hawajaondoka na Kim akamuacha Kanye nyumbani.
Pia inasemekana Kanye alishawahi wafukuza wanaume kazini kwa Kim kardashian kwa sababu ya wivu na kudai kua ni “mahandsome” kupitiliza. Badala yake alibadilisha wafanyakazi hao na kuwaweka wanawake na wanaume mashoga akidai kua mke wake ni mzuri sana kwa wanaume kutomsumbua.
Hii ni wazi Kanye amekua akimpelekesha sana mke wake huyo na kutaka awe juu yake katika kila kitu. Kim analalamika kwani Kanye West anawafanyakazi warembo na wala hajawahi kuingilia kazi zake lakini kwanini yeye ndo aingiliwe na kazi zake?
Licha ya hayo yote inasemekana pia mwanamuziki huyo amekua akitumia hela za mkewe ovyo akidai ana mawazo ya mafanikio lakini mwisho wa siku mawazo yake hayo hayafiki popote.Hatimae Kim yupo hatua chache tu kumpa talaka Kanye ili kuinusuru familia yake.
Kwani siku haiwezi isha bila wa wili hawa kugombana. Kim yupo tayari kupigania watoto wake Saint na North na anaogopa hata kumuacha Kanye na watoto kwa sababu ya ukali wake na hasira,ripoti zilisema.
Post a Comment