Tukiachana na “TV SHOW’ ya ukoo wa “The Kardashians” ijulikanayo kama “Keeping Up With The Kardashian”, mdogo wake na Kim Kardashian ajulikanae kama Rob Kardashian pamoja na mama kijacho wake Blac Chyna, wameamua kuandaa kipindi chao ambacho kitarushwa katika stesheni ya E!.
Rob Kardashian mwenye miaka 29 amekua akiogopa sana kuwepo mbele ya kamera lakini sasa ameamua kuondoa woga huo kwa kutengeneza kipindi chao akiwa na mchumba wake Blac Chyna mwenye miaka 27.
Lakini pia katika kipindi hicho sehemu “exclusive” za kusherekea ukaribisho wa mtoto mpya kutoka kwa Blac Chyna zitaonyeshwa .Tamthilia hiyo itahusisha maisha ya ndani ya wachumba hawa, na mkanda mzima wa jinsi walivyo vishana pete za uchumba na upataji mimba na kila kitu kinacho wahusu Rob & Chyna.Pia katika tamthilia utaonyeshwa mfululizo wa maandalizi ya kumkaribisha mtoto wao wa kwanza na kuanza maisha yao mapya.
Mfululizo huu wa tamthilia utaandaliwa na watayarishaji wa huko Marekani Ryan Seacrest & Bunim na itakua ni matukio sita yakionyeshwa hewani ndani ya lisaa limoja kuanzia mwishoni mwa mwaka huu.
Mwezi wa pili Rob na Chyna walikua bega kwa bega wakifanya makutano kwa masaa mawili na watayarishaji wa tamthilia katika ofisi za Beverly Hills. Makutano hayo yalikuwa yakimuhusisha muandaaji ambaye alishatajwa hapo awali Ryan Seacrest pamoja na kikundi chake kizima. Rob alimchagua mtayalishaji huyo kutokana nakuona kazi zake katika tamthilia ya familia yake “ Keeping up with the Kardashian” na alipenda kazi zake kuanzia hapo.
Tamthilia hiyo inaweza aandaliwa kwa haraka sana na kurushwa katika channel kubwa ya E! Makamu Mtendaji wa channel ya E! alisema kua ni mara chache sana amekua akiona mapenzi ya kweli kufika hatua ya Rob na Chyna, na anafurahi kumuona Rob na Chyna kufikia hapo walipo.Tunafuraha kushirikiana nao katika mahusiano yao, alimalizia kwa kusema hivyo.
Kwa kawaida katika tamthilia hii waandaaji watakua ni pamoja na Ryan Seacrest, Kris Jenner, pamoja na Rob & Chyna.
Post a Comment