Kuanzia muonekano na kufananishwa unaweza kusema Shilole amepata mpinzani! Si mpinzani wa kawaida kama wengine bali ni msichana anayefanana naye kama pacha wake.
Tambua kwamba model huyo anaitwa Zena na ikumbukwe kuwa jina halisi la Shishi ni Zuwena Mohamed!
Ni kama vile wawili hawa walipotezana siku ya kuzaliwa.
Anyway turejee kwenye pointi ya msingi. Unakumbuka Shilole aliwahi kudai kuwa yeye ndiye muimbaji wa kike mrembo kuliko wote Bongo? Zena aka Jike Shupa hakubaliani na hilo.
“Kwakweli mimi namuona wa kawaida tu,” Zena aliiambia Clouds E. “Akumbuke na mimi mzuri kuliko yeye,” aliongeza kwa madaha.
Tangu video ya wimbo huo itoke, uadui kati ya Nuh Mziwanda na Shilole umeongezeka maradufu. Nuh ameitumia video ya wimbo huo aliomshirikisha Alikiba kuonesha jinsi uhusiano wake na Shishi ulivyokuwa na matatizo ikiwemo kupigwa mara kwa mara na Shishi hajapenda!
Post a Comment