Rapper Kiernan Jarryd Forbes, maarufu kama AKA na staa wetu Nasibu Abdul aka Diamond Platnumz wameingia location kushoot video ya collabo yao.
Taarifa ya kufanyika kwa video hiyo imetolewa na AKA kupitia akaunti yake ya Twitter jana Jumapili.
IKISEMA HIVII
In other news: Off to shoot this video for this AKA X @diamondplatnumz collaboration. 🎥💎
— AKA (@akaworldwide) November 29, 2015
Inavyoonekana video hiyo inashutiwa Afrika Kusini kwasababu Diamond Platnumz yuko huko toka wiki iliyopita.
AKA na Diamond walipata nafasi ya kuingia studio kufanya collabo mwezi May mwaka huu, wakati rapper huyo alipokuja Tanzania kwenye Zari All White Party kwa mwaliko wa Diamond.
Post a Comment