0


Industry nzima ya Bongo Flava ilihamia Johannesburg, Afrika Kusini wikiendi iliyomalizika. 
Mwana FA, Diamond, Chege, Julio na mshkaji wakiwa SA

Diamond, Mwana FA, Chege, Shaa, Master J, Julio walikutana jijini humo huku kila mmoja akionekana kwenda kutengeneza video yake. 
Chege, Sallam, Shaa, Godfather na Julio

Kuna kila dalili kuwa Diamond ameenda kushoot video yake mpya na Godfather na huenda mastaa hao wakaonekana kwenye video hiyo. 
Diamond na Chege

Shaa pia ameenda kushoot video mpya japo hakuna uhakika kama ameamua kumtumia Godfather pia au amerudi kwa Justin Campos aliyeshoot video ya wimbo wake Toba. 
Chege, Zari, Shaa na Master J

“Wakati #TOBA inafanya yake…mambo mengine yanasukwa.. @sallam_sk @i_am_godfather @chegechigunda @juliobatalia,” ameandika Shaa.

Mwana FA yupo nchini humo kwa siku kadhaa sasa na tunafahamu kuwa ameshashoot video yake japo kuna uwezekano amebakia kufanya nyingine tena.
Chege na Julio nao wamekuwa huko kwa muda sasa na hivi karibuni walionekana kuwa karibu na Justin Campos kupika kichupa kipya.

Post a Comment

 
Top