Inasemekana kuwa Beyonce yupo tayari kulichukua tena taji lake la malkia wa tasnia ya muziki duniani.
Kwa mujibu wa ripoti, muimbaji huyo atatangaza album yake ya kushtukiza na ziara ya dunia wiki chache zijazo. Inaaminika kuwa muimbaji huyo mwenye umri wa miaka 34 anapanga kuachia santuri mpya kwa kushtukiza baada ya kutumbuiza kwenye mapumziko ya Super Bowl, February 7.
Album hiyo itakayokuwa ya sita, inadaiwa kuwa tayari tangu mwishoni mwa mwaka jana. Hata hivyo Bey alidaiwa kusubiri kwanza kutokana na ushabiki uliokuwepo kwenye album ya Adele, 25 iliyotoka November.
Timu yake iliamini isingekuwa vyema album ya Bey igongane na ya Adele kwakuwa waliamini ni muda wa kung’ara wa msanii huyo wa Uingereza.
Na sasa kwakuwa mauzo ya Adele yameanza kupungua, Beyonce yupo tayari kutoa album yake muda wowote.
Post a Comment