DiamondPlatnumz Aingia Studio Kurekodi Na Producer Wa Norway aliyetengenza wimbo ulioshinda tuzo za Grammy
Diamond Platnumz ameingia studio kurekodi wimbo na producer wa Norway, Carl Hovind aliyekuja Tanzania kama sehemu ya kutafuta ladha tofauti za Afrika ili kuzitangaza duniani.
Hovind yupo nchini kwa wiki kadhaa sasa na amekuwa akikutana na watayarishaji na wasanii wakubwa na wadogo ili kuangalia uwezekano wa kufanya nao kazi.
Mtayarishaji huyo huyo ni mkubwa nchini Norway na mwaka 2014 alitengeneza wimbo wa wasanii wa nchini humo ulioshinda tuzo za Grammy.
Diamond na Carl wamefanya kazi kwenye studio za Wasafi Records usiku wa kuamkia Jumamosi hii. Pamoja na Diamond, Carl aliiambia amesema kuwa wiki hii kuwa anapenda kufanya kazi na Alikiba, Vanessa Mdee, Shaa na wasanii wengine.
Unaweza Kubofya Play Kusikiliza
Unaweza Kubofya Play Kusikiliza
Post a Comment