0


Star wa Bongo Flavor Madee jana aliahidi kuchoma moja ya gari lake endapo timu ya Chelsea ingeifunga Arsenal kwenye mchezo wa Premier League jana January 24 kwenye uwanja wa Emirates.

Mchezo huo ulimalizika kwa Arsenal kukubali kipigo cha goli 1-0 lilifungwa na Diego Costa dakika ya 23 kipindi cha kwanza na kudumu kwa dakika zote za mchezo huo.

Wadau mbalimbali walikuwa na hamu ya kujua kama Madee alitimiza azma yake ya kulitia kibiriti gari lake baada ya Chelsea kuituliza Arsenal kwenye uwanja wake wa nyumbani na kuendeleza rekodi ya kutopoteza mechi nyingi za ligi dhidi ya mahasimu wao wa jiji la London.

Leo asubuhi Madee ame-post ujumbe kwenye account yake ya tweeter akijibu maswali mengi kuhusu matokeo ya mechi ya Arsenal vs Chelsea na yeye kuchoma gari lake.

Star huyo ameandika ujumbe unaosomeka hivi: “Sina utajiri huo mpaka kufikia hatua ya kuchoma gari. Hata kama ningekuwa tajiri vipi, nisingefanya upumbavu huo”.

Jana Madee hakupokea simu ambazo alikuwa akipigiwa na wadau mbalimbali wakitaka kujua kama ametekeleza ahadi yake ya kuchoma gari aliyoitoa kabla ya mchezo huo.
Jana kupitia account yake ya instagram Madee alipost ujumbe kwamba, endapo Chelsea ikiifunga Arsenal atachoma moto gari lake moja.

Credit To shaffi

Post a Comment

 
Top