0

Staa wa soka wa kimataifa wa Brazil Ronaldinho Gaucho bado yupo kwenye headlines, licha ya kuwa hayupo katika timu kubwa ambazo tumezoea kumuona, lakini uzito wa jina lake bado ni mkubwa katika medani za soka, staa huyo aliyejijengea umaarufu mkubwa akiwa katika vilabu vya PSG na FC Barcelona amenusurika kupata ajali leo January 25 India.

Ronaldinho alipata nafasi ya kualikwa katika uzinduzi wa mashindano ya soka ya Sait Nagjee ambayo yalikuwa yanafufuliwa tena baada ya kutofanyika kwa takribani miaka 20 sasa, umati mkubwa ulikusanyika kumshuhudia Ronaldinho ambaye wamekuwa wakimuona katika tv kwa muda mrefu.

Kutokana na umati mkubwa uliokuwa umekusanyika barabarani, Ronaldinho wakati anaondoka akiwa ndani ya gari nusura bomba linaloshikilia taa za barabarani liangukie gari aliyokuwa kapanda, tukio ambalo lilisababisha na umati wa watu. Unaweza kutazama video zenyewe mtu wangu.

Post a Comment

 
Top