Ni kawaida kwa vilabu vya soka barani Ulaya kuwa na utamaduni na mbinu tofauti tofauti za kuhakikisha kila mwaka wanaendeleza kuiingizia klabu mapato, moja kati ya mbinu zinazotumika kuiingizia klabu mapato ni kubuni muonekano wa jezi mpya kila msimu pasipo kubadili rangi husika za klabu ili shabiki avutike kununua kila msimu.
![]() |
jezi za ugenini watakazotumia msimu wa 2016/2017 |
April 26 2016 stori kutoka mtandao wa 101greatgoals.com wameonesha jezi mpya za Arsenal zitakazotumika msimu wa 2016/2017, jezi hizo za Arsenal hazijatolewa wala kutangazwa rasmi na klabu hiyo bali zimevuja kutoka vyanzo vya ndani ya klabu hiyo na bado zitaendelea kutengenezwa na Puma kama kawaida.
![]() |
muonekano wa jezi mpya za nyumbani watakazotumia msimu wa 2016/2017
Credit MillardAyo
|
Post a Comment