0


Mwanadada Kylie Jenner ambae pia ni EX wa rappa Tyga ameonekana kumsahau kabisa Tyga licha ya kua ni wiki kadhaa sasa  tangu wapenzi hao kuachana. 

Kylie Jenner anasadikika kupata mpenzi mpya anaekwenda kwa jina la “PARTYNEXTDOOR”au kwa kifupi PND na hilo sio jina lake la kuzaliwa.
PARTYNEXTDOOR pia ni mwanamuziki na alishafanya nyimbo na Drake inayokwenda kwa jina la “Recognize”.  Chanzo chetu cha habari E! News kimepata tetesi kua Kylie na PND ni marafiki tu.

 Yawezekana Kylie bado yupo kwenye harakati za kusahau mahusiano yake na rappa Tyga na kutaka kujiandaa kwa ajili ya msimu wa “summer” ( msimu wa jua) bila kua kizuizi chochote.
Yote hii imetokana na picha iliyowekwa Instagram na “PARTYNEXTDOOR” ikiwa na mikono miwili tofauti (mmoja ukiwa ni wa Kylie” na kisha kuweka caption “Diamond battles with @kyliejenner” ikiwa inamaanisha “mapambano ya diamond” kisha kumtag mrembo huyo.

 Hapo ndipo maswali yalipoanza kuzuka kwani ilionekana wazi kua Ex wa Kylie, Tyga alionekana kua na wivu na post hiyo iliyowekwa na Instagram, na siku moja baadae na yeye Tyga aliweka picha ikiwa na saa zake na pete  za diamonds na kisha kuweka maneno yale yale “Diamond battles”

Credit To Eye De Marie

Post a Comment

 
Top